Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web

  BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIM:{In The Name Of Allah,The Beneficient,The Merciful}
     
NYUMBANI

KUHUSU KURASA

PICHA

NINI KIPYA

ANWANI

VIUNGANISHI CHAGUO

MAKALA NA PICHA 1

MAKALA NA PICHA 2

MAKALA NA PICHA 3

MAKALA NA PICHA 4

MAKALA NA PICHA 5

MAKALA NA PICHA 6

MAKALA NA PICHA 7

MAKALA NA PICHA 8

MAKALA NA PICHA 9

MAKALA NA PICHA 10

 
ASSALAAM ALEYKUM: {Peace Be Upon You}

 

UISLAMU.

Uislamu ndio dini ya maumbile bila ya makindano. Yaani Uislamu ndio mfumo wa maisha unaokwenda sambamba na maumbile ya mwanadamu na ulimwengu wake. Kwa mantiki hii tunaweza kusema kwa kinywa kipana kabisa kwamba Uislamu ndio dini ya jamii ya wanadamu. Uislamu haukuitwa dini ya jamii ya wanadamu kwa kuropoka tu au kwa hamasa na jazba. Imeitwa hivyo kwa sababu zifuatazo:-
1. Imesheheni desturi zinazokubaliana na akili.
2. Ina uongofu unaouangazia na kuupa nuru moyo.
3. Inabeba maendeleo yanayofaa kwa hali, mahala na zama zote.
4. Ina sheria inayokidhi hali na mahitaji yote ya jamii katika nyanja zote za maisha.
5. Ina dhana ya usawa unaowaunganisha pamoja watu wote bila ya kujali lugha, rangi au hali zao za kimaisha.
6. Sheria yake ina dhima ya kumpa mwanadamu maisha ya amani, utulivu, raha, furaha na heshima katika nafsi, mwili, akili na mali.
Haya na mengineyo ndiyo yanayoufanya Uislamu uwe ni dini inayokubaliwa na kuridhiwa na mwanadamu kwa kuwa inayogusa moja kwa moja maumbile yake.

MAZINGATIO KATIKA DINI:

Kila nafsi itaonja mauti. Na bila shaka mtapewa ujira wenu kamili siku ya kiama. Na aliyewekwa mbali na moto na akaingizwa peponi basi amefuzu. Maisha ya duniani si kitu ila ni starehe idanganyayo. {3:185}Na maisha ya dunia si kitu ila ni mchezo tu na upuuzi. Na bila shaka nyumba ya akhera ni bora zaidi. Basi hamtii akilini. {6:32}
Popote mlipo mauti yatakufikieni, hata mkiwa katika ngome madhubuti.{4:78}
Kukimbia hakutakufaeni kama mkikimbia mauti au kuwa katika vita, na kwa hivyo [hata mkikimbia]hamtaishi ila kidogo [kasha mara mtakufa]{33:16}
2:255
2:177
Mtume {s.a} amepewa mambo matano ambayo hawakupewa mitume wenzie waliopita.

  • Ameondolewa woga
  • Amehalarishiwa ardhi iwe tohara {haina najisi unaweza kusali mahali popote katika ardhi}Maana watu wa awali walikuwa na sehemu maalum kwa ajili ya swala.
  • Amehalarishiwa ngawila {mali zinazopatika vitani ni hali kwetu}
  • Amepewa uombezi kwa waumini {atakuwa ni mwenye kuwaombea waumini katika umma wake msamaha kwa Mwenyezi Mungu}
  • Ameletwa kwa ajili wa watu wote.


    UMUHIMU WA KUSHIKAMANA NA TABIA NA UTAMADUNI WA KIISLAMU:
    Lazima tufahamu kwambakuendelea kuwepo kwetu{sisi Waislamu} kama ambavyo kunategemea kuwepo kwa itikadi za Kiislamu vile vile kunategemea kuwepo kwa tabia na maadili ya Kiislamu. Kuna uhusiano mkubwa na wa ndani sana kati ya itikadi na tabia. Kuwepo kimoja wapo kunalazimisha kuwepo kingine.
    Itikadi ya Kiislamu ndiyoinayotutaka tuwe na tabia na maadili maalum. Sisi Waislam hatuwezi kuendelea kupata heshima hapa ulimwenguni ila tu kwa kufuata misingi ya tabia na maadili yaliyoletwa na Uislam,maadili ambayo Alla{s.w} na Mtume wake {s.a.w} wametuongoza.



Mtume wa Allah {s.a.w} alipo kwenda safari yake ya Israa, aliwakuta Wanawake wengi sana wako Motoni. Akauliza sababu ya kuwepo kwao Motoni kwa wingi, akajibiwa kwa kutajiwa sababu nyingi tu mojawapo zikiwa ni hizi; 1. Kwa kuwa wamekuwa watu wa kunung'unika sana[wanung'unikaji sana]
2. Hawalidhiki na walivyonavyo Waume zao.
3. Wanazikufuru neema wanazoneemeshwa na Mola wao.
Kwa hiyo wanatakiwa waepukane na hayo na kama wanayo mambo hayo wanatakiwa watoe Sadaka kama Toba kwao.
Toba ni kitu muhimu kwa mwanadamu yeyote kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu na ina faida kubwa na ni muhimu kwa mujibu wa Qur'ani.
66:8, 73:20, 25:70-71, 16:119, 6:54 na 39:53.


MTIZAMO WA UISLAMU JUU MAANA YA DINI:
Mtizamo wa uislam juu ya maana ya dini unatofautiana na ule wa kikafiri katika nyanja mbili {2} a) Si lazima mtu amwamini Mwenyezi Mungu au miungu walio shirikishwa naye ndiyo awe na dini.
b) Makafiri nao wana miungu wanaowafuata.
2. Vile vile Uislamu umeigawanya dini katika makundi makuu mawili.
a) Itikadi au mfumo wa maisha.
b) Siku ya malipo au maisha baada ya kufa.
3. Makafili wanadai kuwa mwanadamu anaweza kuishi bila ya dini na ni bora kufanya hivyo Chimbuko la dai hilii:ni kutokuelewa maana halisi ya DINI, chanzo au Asili ya dini na kazi ya dini katika jamii.Udhaifu wa Dai hili: Ni kwamba mtu hawezi kwa namna moja au nyingine kuishi bila ya Dini, ukizingatia maana halisi ya neon dini ni Itikadi au Mfumo wowote wa maisha unaomwongoza mtu katika maisha yake ya kila siku, ndiyo dini yake.
4. Tofauti ya mtazamo wa makafiri juu ya dini na wale wenye itikadi ya kugawanya maisha katika maisha ya Dunia na Dini. NI KWAMBA makafiri dini kwao inamrudisha binadamu nyuma kimaendeleo, kwa hiyo dini kwao haina umuhimu wowote. Wakati wenzao wanao gawa maisha ya dini na maisha ya dunia, Dini kwao haihusiani na maisha ya kila siku, ila dini inahitajika kwao kwa ajili ya kumfrahisha Mwenyezi Mungu au Kumwomba mambo yaliyo nje ya uwezo wa kibinadamu.
UKILINGANISHA: Wote kwa pamoja wanajikuta wanamuhitaji Mwenyezi Mungu kwa namna moja au nyingine katika kuyaendesha maisha yao ya kila siku.
5. Ukijadili kwa kina mwanadamu hawezi kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine kutokana na maana halisi ya neneo dini umbile lake na vipawa vya hali ya juu alivyotunukiwa na Mwenyezi Mungu Muumba utapata jibu zuri sana.
6. Kwa kuzingatia maana halisi ya neon Dini na kwamba hapana nafasi ya mtu kwa mtu kufuata dini mbili kwa wakati mmoja. Ukijadili kwa kina juu ya dini ya wale wajiitao waislamu lakini mwongozo wao wa maisha yao ya kila siku ni nje ya mwongozo wa Qur'an na sunnah,
Hawa watakuwa bado wana dini lakini mwongozo wao ni kuziendekeza nafsi zao {matamanio}. Matokeo yao ni kwenda kinyume na utaratibu wa maisha aliouweka Mwenyezi Mungu[sw]
AFANYAE UBAYA HATALIPWA ILA SAWA NA HUO UWOVU WAKE NA AFANYAE WEMA AKIWA MWANAUME AU MWANAMKE NAYE NI MWISLAMU, BASI HAO WATAINGIA PEPONI WARUZUKIWE HUMO BILA HISABU{40:40}



Jinsi ya Kuswali.


Jukumu la kujitwika:
Jukumu lililopo ni la Mashekh, Maulamaa na Waalimu wa Ulimwengu kwa ujumla kuwaelimisha vijana kuhusu misingi ya maadili ya Uislamu.
Maadui wa Uislaamu wanajaribu sana kuwapoteza vijana wetu, wana lengo la kuwafanya wasifuate miongozo ya kiislamu ili kuwatoa katika Uislaamu.
Na wewe unatakiwa uwe mmoja wapo katika jukumu hilo, usiwe nyuma katika hilo la kutoa Elimu ya maadili ya Uislamu kwa kidogo ulicho nacho, usijiegemeze unapotukanwa UISLAMU.Wala usiwe katika hao wanao potoshwa na makafiri.

Uislamu ni Dini iliyojengwa juu ya misingi ya haki kwa ajili ya ukombozi wa Mwanaadamu na ni dini inayolenga maswala yote ya Jamii bila ya kubagua tabaka la watu wala rangi ndiyo maana makafiri wanaipiga vita sana.

MWISHO ZINGATIA HILI:
Lau kama hili ni neno lililozoeleka sana miongoni mwa wanaadamu wanapofikwa na dhara au kitu chochote ambacho nafsi yake haipenderei, basi hulitamka kwa wepesi. Haiswihi kutumia neno kwa anayemwamini Allah{sw} anapofikwa na ambacho nafsi yake isichokipenderea au dhara lolote kwa ujumla. Kwani neno hili {Lau kama} linafungua mlango wa Shetani. Ila kwa aliye muumini wa kweli anatakiwa atumie neno "ALOTAKA MWENYEZI MUNGU LIMETIMIA"

*****Tumtaje Mwenyezi Mungu kwa wingi huenda tukawa ni wenye kufaulu.*****

Uislamu:
 
   
 

2:208. Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za She'tani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.